1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miili ya watu 8 yagunduliwa kwenye dampo la takataka Nairobi

Angela Mdungu
14 Julai 2024

Jeshi la polisi nchini Kenya limesema kuwa miili ya wanawake 8 iliyokuwa kwenye dampo katika eneo moja la makazi duni imepatikana jijini Nairobi.

Maafisa wa usalama wa Kenya
Maafisa wa usalama wa KenyaPicha: Brian Inganga/AP Photo/picture alliance

Jeshi hilo limeongeza kuwa kwa sasa linachunguza ili kupata uhusiano kati ya tukio hilo na masuala ya imani za kidini, wahalifu wanaofanya mauaji ya kupanga au watoa huduma za afya kinyume cha sheria.

Katika tukio hilo la kutisha, miili ya wanawake hao ilipatikana ikiwa imekatwa katwa na kufungwa kwenye mifuko ya plastiki kwenye sehemu iliyojaa takataka eneo la Mukuru, kusini mwa mji mkuu wa Nairobi.

Soma pia: Polisi wachunguzwa kuhusu miili iliyokutwa imetupwa Kenya

Kaimu Mkuu wa jeshi la polisi la Kenya Douglas Kanja amesema kuwa miili sita ya kwanza ilipatikana Ijumaa, na miili mingine ilipatikana jana Jumamosi. Kanja ametoa wito kwa wananchi kuonesha ushirikiano ili kufanikisha kuwapata wahusika wa unyama huo na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW