1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi Kenya yazuia mkutano wa wanaharakati na wanahabari

30 Oktoba 2023

Maafisa wa polisi nchini Kenya wamezuia mkutano wa waandishi habari Jumatatu uliokuwa na lengo la kukusanya na kuripoti kuhusu madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanywa na wanajeshi wa Uingereza nchini humo.

Maafisa asiopungua 20 walifika kwa lori na kuzuia mkutano wa wanaharakati usifanyike Kenya.
Maafisa asiopungua 20 walifika kwa lori na kuzuia mkutano wa wanaharakati usifanyike Kenya.Picha: Thomas Mukoya/REUTERS

Kabla ya kufanyika mkutano huo maafisa wasiopungua 20 walifika kwa lori na kuzuia usifanyike.

Hatua hiyo imechukuliwa ikiwa ni saa chache kabla ya mfalme Charles wa Uingereza kuwasili kwa ziara ya siku nne nchini humo.

Wakaazi wa eneo la Lolldaiga katika eneo la kati mwa Kenya wamekituhumu kikosi cha Uingereza cha mafunzo ya kijeshi kilichoko karibu na eneo hilo, kwamba kilihusika kusababisha moto wa msituni mnamo mwaka 2021, ulioharibu eneo kubwa la ardhi ya hifadhi ya mazingira na kuacha zana za kijeshi zilizo sababisha majeraha kwa wakaazi wa eneo hilo.

Wamedai pia wamehusika na mauaji ya mwanamke aliyeonekana mara ya mwisho akiwa na wanajeshi wa Uingereza.

Uingereza iliwahi kuahidi kuchunguza madai hayo dhidi ya kikosi chake hicho chenye wanajeshi takriban 100.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW