1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano ya kuipinga serikali kufanyika Korea Kusini

6 Desemba 2024

Makumi kwa maelfu ya watu nchini Korea Kusini wanatarajiwa kufanya maandamano kesho Jumamosi kumpinga Rais Yoon Suk Yeol.

Korea Kusini
Maandamano makubwa ya kuipinga serikali yanatarajiwa Korea KusiniPicha: Ahn Young-joon/AP Photo/picture alliance

Waandaaji wa maandamano hayo wamesema wanakadiria kuwa takriban watu 200,000 watashiriki maandamano hayo.

Polisi mjini Seoul imesema katika taarifa kuwa maelfu ya watu watafanya maandamano katikati mwa mji huo na eneo la Yeouido na kwamba itaweka vizuizi katika baadhi ya barabara.

Mkuu wa chama tawala Korea Kusini 'amgeuka' rais

Mnamo siku ya Jumanne, Rais Yoon alitangaza sheria ya kijeshi kabla ya kulazimishwa kuubadili msimamo wake baada ya wabunge kupiga kura kuipinga sheria hiyo.

Upinzani umewasilisha hoja ya kumuondoa madarakani Yoon Suk Yeol ambayo inatarajiwa kupigiwa kura kesho Jumamosi, huku kiongozi wa chama cha Yoon akishinikiza rais huyo avuliwe madaraka.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW