Polisi Marekani yaua rai wa asili ya kiafrika
12 Mei 2015Mitindo ya kuwapiga hadi kufa na kufyetuliwa risasi raia wa kimarekani wenye asili ya kiafrika au kilatini,na hasa wanaume,na polisi imekuwa ikiendelea. Mtindo mmoja na kisa cha hivi karibuni kilichotangazwa kwa mapana na marefu, ni kile cha Fredie Gray kilichotokea Baltimore Maryland.Gray aliyekuwa na umri wa miaka 25, alifariki April 19 kutokana na mjeraha ya kile kinachotajwa kuwa "mauwaji". Baada ya kushikiliwa kwa tuhuma kukutikana na kisu mfukoni bila ya ruhusa.Maafisa sita wa polisi wanatuhumiwa kuhusika na kuuliwa kijana huyo.
Wimbi la kadhia kama hizo ambazo nyingi zimenaswa katika kamera na kuoneshwa katika mitandao ya kijamii limezusha malalamiko kote nchini Marekani, na kuanzishwa kampeni iliyopewa jina "kadhia ya maisha ya weusi."
Novemba 28 mwaka mmoja baada ya kamati inayopambana na mateso kuchapisha ripoti kali dhidi ya visa kama hivyo,Marekani ilitakiwa itoe maelezo ya kile inachofanya kujibu mapendekezo yaliyotolewa. Ikiwa ni pamoja na kufanywa haraka uchunguzi na kuandaamwa kisheria visa vya matumizi ya nguvu vinavyofanywa na polisi, pamoja na kupatiwa fidia na tiba wahanga wa matumizi hayo ya nguvu.
"Njia bora zaidi ya kukomesha ubaguzi na hasa mauwaji ya polisi ni kwa kile tunachokiona hivi sasa:maandamano makubwa ya wanaharakati katika kila pembe ya Marekani" Michael Ratner,mwenyekiti wa shirika la Emeretus linalopigania haki za kikatiba shirika lenye makao yake mjini New.York ameliambia shirika la habari la IPS."Tuko katika wakati wa aina pekee kwa kile ambacho ni nadra kutokea nchini;watu wamevinjari na wanateremka majiani.Huu ndio ufunguo.Miji yetu haiwezi kutawaliwa bila ya ridhaa ya wanaotawaliwa."
"Lakini bila ya shaka kuna mengine ambayo ni muhimu pia.Mtandao wa tume ya Umoja wa mataifa dhidi ya mateso UN CAT unawapatia nafasi wamarekani wenye asili ya Afrika, kuzungumzia kilicho muhimu hasa-kwa maneno mengine kile kilicho na umuhimu mkubwa zaidi.Mtandao huo umeipatia familia ya Michael Brown, uwanja wa kusikika kote ulimwenguni,sawa na walivyofanya wengineo.Maoni ya tume hiyo ya UN CAT ni makali na katika wakati ambapo Marekani inajaribu kuyapuuza,ulimwengu unajibu.Ripoti ya shirika hilo la Umoja wa mataifa, inahalalisha maandamano hayo yanayotokea kila kukicha.
Michael Brown alikuwa mmarekani mweusi kijana ambae hata silaha hakua nayo,alipigwa risasi na kuuliwa na polisi mmoja Mmarekani mweupe Darren Wilson huko Ferguson-Missouri.Jopo la majaji wamekataa kutoa uamuzi kijana huyo mdogo, alipouwawa Agosti 9 mwaka 2014.
Wazee wa Brown walitoa ushahidi wao mbele ya tume hiyo ya Umoja wa mataifa mjini Geneva mwaka jana, na mkuu wa halmashauri ya Umoja wa mataifa inayoshughulikia haki za binaadam Zeid Al Hussein alizungumzia kesi hiyo na kulaani kile alichokiita "ubaguzi unaohalalishwa kisheria" nchini Marekani.
Mwandishi: Hamidou Oummilkheir/IPS
Mhariri:Yusuf Saumu