1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi na Wanajeshi wavamia makazi ya wakimbizi kusini mwa Khartoum.

25 Mei 2005

Maelfu ya askari polisi wenye silaha wakiambatana na wanajeshi,wamefanya uvamizi katika kambi kubwa inayohifadhi wakimbizi wa Sudan,kusini mwa mji wa Khartoum.

Operesheni hiyo iliwashirikisha wanajeshi 6,000 na maofisa wa polisi 400,ambao waliizingira kambi hiyo,iliyopo kilometa 30 kusini mwa mji mkuu Khartoum na kuwakamata watu 50,ambao wanawahusisha na mauaji ya askari polisi 17, waliouawa wakati wa machafuko ya wiki iliyopita.Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi wa mji wa Khartoum,watu wengine 32 walitiwa mbaroni kutokana na vitendo vya uporaji na kukitia moto kituo cha polisi katika kambi hiyo.

Vibanda na kambi vinavyouzunguka mji wa Khartoum ni makazi ya zaidi ya watu milioni 2,wengi wakiwa wanatoka maeneo ya kusini ambao walikimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miongo miwili.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW