1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaArmenia

Waandamanaji 226 wakamatwa Armenia

27 Mei 2024

Armenia imesema kuwa polisi nchini humo imewakamata zaidi ya waandamanaji 200 wanaomtaka Waziri Mkuu Nikol Pashinyan ajiuzulu.

Armenia | Waandamanaji kwenye mji wa Yerevan
Polisi wakiwa wamemkamata mmoja ya waandamanaji wanaoipinga serikali ya Nikol PashinyanPicha: Hayk Baghdasaryan/Photolure/AP/picture alliance

Waandamanaji hao wanamtaka Pashinyan aachie ngazi kutokana na hatua yake ya kukubali kuiachia sehemu ya ardhi kwa taifa hasimu la Azerbaijan.

Taarifa ya wizara ya usalama wa ndani inasema kuwa watu 226 wanashikiliwa na polisi kwa kutotii amri ya polisi.

Msimamo wa Pashinyan bado haujabadilika licha ya upinzani ulioanzishwa na askofu mkuu Bagrat Galstanyan anayejaribu kuanza mchakato wa kumuondoa madarakani.

Mamia ya waandamanaji wameingia mitaani kote Armenia wakijaribu kuweka vizuizi barabarani katika kile ambacho Galstanyan amekiita "kampeni ya nchi nzima ya kutotii."

Wiki iliyopita Armenia ilirudisha udhibiti wa vijiji vinne vya mpakani ilivyoviteka kutoka kwa Azerbaijan miongo kadhaa iliyopita, hatua muhimu katika kurejesha mahusiano baina ya nchi hizo mbili ambazo zimepigana vita miaka ya karibuni.