1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroHaiti

Haiti: Polisi waendelea kukabiliana na magenge ya wahalifu

17 Machi 2024

Polisi nchini Haiti wanaendelea kukabiliana na magenge ya wahalifu ambayo yamesababisha mtafaruku katika nchi hiyo ya Caribbean.

Haiti- Uhalifu wa magenge yenye silaha
Polisi wa Haiti wakijaribu kuimarisha ulinzi wakati wa msafara wa lori za mafuta mjini Port-au-PrincePicha: Odelyn Joseph/AP/dpa/picture alliance

Polisi wamesema wamefanikiwa kuondoa vizuizi na kuwaua majambazi kadhaa wakati wa operesheni yao katika mtaa wa Delmas.

Hata hivyo vurugu zinaendelea katika mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince ambako magenge yanadhibiti asilimia 80 ya mji huo. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia watoto UNICEF limesema moja ya kontena lake lililokuwa limebeba vifaa muhimu liliporwa na magenge katika bandari kuu ya Haiti.

Soma pia: Hofu yatanda Haiti katikati ya mkwamo wa kisiasa

Shirika la kikanda CARICOM, Umoja wa Mataifa na Marekani wanaunga mkono kuanzishwa kwa baraza la mpito ili kuchukua nafasi itakayoachwa na Waziri Mkuu Ariel Henry, ambaye alitangaza Jumatatu kuwa angejiuzulu mara baada ya kuundwa kwa baraza hilo la kisiasa.