Polisi nchini Morocco wamewakamata watuhumiwa watatu zaidi
20 Desemba 2018Polisi nchini Morocco wamewakamata watuhumiwa watatu zaidi katika mauaji ya watalii wawili wanawake , kutoka Norway na Denmark, katika milima ya Atlas.
Siku moja kabla maafisa nchini Morocco walisema wanawatafuta watuhumiwa wengine watatu baada ya mtu mmoja kukamatwa mjini Marrakech. Mwendesha mashitaka mkuu wa serikali amesema mtu huyo ambaye yuko kizuwizini ni mwanachama wa kundi la wanmgambo, lakini hakutoa jina la kundi hilo.
Miili ya Louisa Vesterager Jespersen mwenye umri wa miaka 24, kutoka Denmark na Maren Ueland , mwenye umri wa miaka 28 kutoka Norway , ilipatikana siku ya jumatatu katika eneo la mbali karibu na Imlil, katika njia kuelekea Toubkal, kilele cha juu kabisa cha milima katika taifa hilo la Afrika kaskazini na eneo maarufu kwa watalii.