Polisi Pakistan yafunga baadhi ya maeneo ya Islamabad
18 Machi 2023Matangazo
Wakazi wa karibu na mahakama itakayosikiliza kesi ya Khan wametakiwa kubaki nyumbani na mikusanyiko ya kisiasa imepigwa marufuku.
Mkuu wa polisi wa Islamabad Akbar Nasir amesema wameweka ulinzi mkubwa wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo ili kuhakikisha kuwa waziri mkuu huyo wa zamani hatishiwi maisha yake.
Soma pia:Mahakama ya Pakistan yazuia Khan kukamatwa
Imran Khan, aliondolewa madarakani baada ya bunge kupiga kura ya kutokuwa na imani naye mwaka 2022. Mahakama mjini humo ilitoa hati ya kukamatwa kwake mwezi uliopita. Khan aliepuka kukamatwa kwa wiki nzima kufuatia vurugu za wafuasi wake.