1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi Uturuki yawakamatwa waandamanaji kadhaa Mei Mosi

1 Mei 2026

Polisi nchini Uturuki wamekabiliana leo na waandamanaji waliojaribu kuelekea kwenye uwanja wa Taksim katikati ya jiji la Istanbul kwenda kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wafanyakazi.

Uturuki Ankara 2026 | Maandamano
Waakilishi wa baadhi ya vyama vya wafanyakazi Uturuki wakutana katika uwanja wa Anadolu kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wafanyakazi mnamo Mei 1, 2026Picha: Arman Onal/Anadolu Agency/IMAGO

Vyama vya ndani vya wafanyakazi pamoja na Chama cha Wanasheria wa Maendeleo (CHD), kimeliarifu shirika la habari la Ujerumani dpa kwamba idadi ya waliozuiliwa ilikuwa zaidi ya 350.

Kulingana na mwakilishi mmoja wa CHD, waandamanaji kadhaa tayari wamefikishwa katika makao makuu ya polisi, huku baadhi wakiripoti kupata majeraha walipokuwa wakipelekwa kizuizini. Hata hivyo idadi kamili ya waliozuiliwa haikuweza kuthibitishwa mara moja.

Nchini Ujerumani, wafanyakazi waliandamana kote nchini humo huku vyama vya wafanyakazi vikilalamika kuhusu mipango ya kupunguza huduma za afya na faida ya usalama wa kijamii.

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini Ujerumani DGB Yasmin Fahimi, amewaambia maelfu ya waandamanaji waliojitokeza kwamba ikiwa watashambuliwa watajilinda na kwamba lazima wabaki kuwa tayari kwa malumbano katika wiki ama miezi ijayo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW