1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAfrika Kusini

Zoezi la uokoaji lakamilika katika mgodi wa Stilfotein

16 Januari 2025

Polisi nchini Afrika Kusini wametangaza siku ya Jumatano kuwa wamemaliza operesheni ya uokoaji katika mgodi wa dhahabu uliotelekezwa wa Stilfotein uliopo kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Polisi wa Afrika Kusini wakielekea kwenye zoezi la uokoaji kwenye mgodi haramu
Polisi wa Afrika Kusini wakielekea kwenye zoezi la uokoaji kwenye mgodi haramuPicha: Christian Velcich/AFP

Takriban wachimba migodi 78 wamethibitishwa kufariki huku manusura 246  wakiokolewa. Makundi ya kutetea haki za binaadamu nchini Afrika Kusini yamesema kuwa idadi ya vifo inaweza kuwa kubwa zaidi na kwamba waathiriwa wanashukiwa kuwa walifariki kwa njaa au upungufu wa maji mwilini, ingawa mamlaka hawajatoa sababu zilizopelekea vifo hivyo.

Soma pia: Takriban watu 100 wafariki, mamia wakwama mgodini Afrika Kusini

Polisi hata hivyo wamesema wanaamini kuwa wamefanikiwa kuwaondoa manusura waliosalia na kuopoa miili yote baada ya mamia ya wachimba migodi kukwama kwa miezi kadhaa katika mgodi huo wenye kina kirefu wakifanya kazi kinyume cha sheria.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW