1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi wa Israel na Wapalestina wapambana tena

10 Mei 2021

Polisi wa Israel wamekabiliana na waandamanaji wakipalestina katika eneo takatifu la Jerusalem ambalo ni kitovu cha vurugu kwa majirani hao wa Mashariki ya kati. Makabiliano hayo yametokea leo Jumatatu.

Israel | Unruhen in Jerusalem
Picha: Ammar Awad/REUTERS

Maafisa walifyetua gesi ya kutowa machozi na maguruneti ya kurusha kwa mkono na waandamanaji wakipalestina kwa upande wao waliwarushia mawe na vifaa vyingine maafisa hao.

Kwa mujibu wa polisi,waandamanaji walirusha mawe kutokea ndani ya uwa wa  msikiti mtakatifu wa Al-Aqsa kuelekea eneo la barabara ya njia panda.

Kwa upande wa wapalestina wamefahamisha kwamba maguruneti yalirushwa kuelekea msikitini na watu kadhaa wamejeruhiwa.

Awali polisi iliwazuia wayahudi kutotembelea eneo hilo hii leo ambapo Waisraeli wanaandhimisha siku ya Jerusalem,tukio linalofanyika  kila mwaka ambalo linatazamwa kwa kiasi kikubwa kama uchokozi wa Israel katika mji huo unaogombaniwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW