1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kitisho cha shambulizi kwa Kanisa Kuu Cologne

2 Januari 2024

Polisi wa Ujerumani wanamshikilia mshukiwa wa tano katika njama ya kanisa kuu la Cologne

Deutschland | Polizeieinheiten am Kölner Dom
Picha: Roberto Pfeil/dpa/picture alliance

Mshukiwa wa hivi karibuni kuzuiliwa kwa madai ya njama ya kushambulia Kanisa Kuu la Cologne ni mwanaume mwenye umri wa miaka 41 Mjerumani mwenye asili ya Kituruki. Polisi wameimarisha kufanyika ulinzi mkali katika eneo hilo la ibada lenye umaarufu mkubwa duniani.

Jana Jumatatu Mamlaka ya Ujerumani ilisema ilimzuia mtu mwingine kuhusiana na njama inayoshukiwa kuwa ya kigaidi kwenye Kanisa Kuu maarufu la Cologne Cathedral, na kufanya jumla ya waliokamatwa kufikia watano.

Mfululizo wa kamatakamata ya washukiwa.

Polisi wakiwa katika juhudi za ulinzi na usalama katika eneo la Kanisa Kuu ColognePicha: Roberto Pfeil/dpa/picture alliance

Mapema, Jumapili, polisi waliwakamata watu wengine watatu ambao waliachiliwa baadaye. Polisi pia walimtia mbaroni raia wa Tajikistan mwenye umri wa miaka 30 siku ya mkesha wa Krismasi. Siku ya Jumatatu, polisi waliongeza muda wa kuwaweka kizuizini washukiwa wawili kwa siku 14 ili wafanyiwe mahojiano zaidi.

Washukiwa wote wanadaiwa kuwa na uhusiano na kundi liitwalo IS-Khorasan, tawi la kundi linalojiita "Dola la Kiislamu" kwa Afghanistan.

Kanisa kuu la Cologne chini ya ulinzi mkali.

Polisi wa Ujerumani wakiwa katika jukumu la kuimarisha usalama katika kanisa la ColognePicha: Ina Fassbender/AFP/Getty Images

Vyombo vya habari vya eneo hilo viliripoti kuwa njama hiyo inayoshukiwa kuwa ya kigaidi ilipaswa kutekelezwa siku ya mkesha wa Mwaka Mpya na gari lililokuwa na vilipuzi.

Soma zaidiPolisi wa Ujerumani waimarisha ulinzi katika Kanisa Kuu la Cologne kufuatia kitisho

Siku ya Jumapili, polisi wa Cologne walisema kuwa eneo la maegesho ya gari ya chini ya ardhi ya kanisa hilo kuu ilipekuliwa na kwamba mbwa wa kugundua viripuzi wametumwa, lakini hakuna kilichopatikana. Siku ya Jumatatu, polisi walisema wataendelea kulinda Kanisa Kuu la Cologne.