1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi wamwagwa India kuwakabili wakulima wasiandamane

13 Februari 2024

Vikosi vya usalama nchini India leo vimetumia mabomu ya kutoa machozi kuwazuia maelfu ya wakulima kuandamana kwenye mji mkuu New Delhi baada ya kusambaratika kwa mazungumzo na serikali kuhusu madai yao.

India | Maandamano ya wakulima
Polisi wa India wakijiandaa kukabiliana na wakulimaPicha: Manish Swarup/AP Photo/picture alliance

Vyombo vya habari vya ndani nchini India vimeonesha wingu zito la moshi wa mabomu ya machozi ukifuka baada ya polisi kuyafyetua walipokuwa wakiwakabili waandamanaji karibu na mji mdogo wa Ambala, umbali wa kiasi kilometa 200 kutoka New Delhi.

Polisi pia wameweka vizuzizi vya nyaya za chuma na zege kwenye njia zote kuu zinazozunguka majimbo matatu yanayokaribiana na mji mkuu.

Miongoni mwa madai mengine wakulima wa nchi hiyo wanaishinikiza serikali kuweka utaratibu wa kutangaza bei elekezi ya mazao. Wakulima nchini India wanayo nguvu kubwa kutokana na wingi wao unaofikia theluthi mbili ya idadi jumla ya watu bilioni 1.4 wa taifa hilo.

Mwaka 2021 walifanya maandamano yaliyoitikisa nchi hiyo na kuilazimisha serikali kubadili sheria kadhaa zilizozusha malalamiko.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW