Polisi waombwa kumkamata rais wa Korea Kusini
6 Januari 2025Ombi hilo ni baada ya maafisa wake kushindwa kumuweka kizuizini kufuatia makabiliano ya masaa kadhaa na walinzi wa rais huyo wiki iliyopita.
Ofisi hiyo na jeshi la polisi zimethibitisha kuzungumzia suala hilo hivi leo, yakiwa yamebakia masaa machache kabla ya kumalizika kwa muda wa waranti wa wiki moja uliotolewa na mahakama.
Soma zaidi:Maelfu ya waandamanaji Korea Kusini wakusanyika Seoult
Ofisi hiyo huenda ikaiomba mahakama kuipa waranti mpya wa kuongeza muda wa kumuweka Yoon kizuizini, kwa mujibu wa polisi. Mahakama ya Wilaya ya Seoul Magharibi ilikuwa imetowa waranti wa kumkamata Yoon mnamo tarehe 31 Disemba, baada ya kukwepa miito kadhaa ya kujitokeza kuhojiwa.
Ofisi ya kupambana na ufisadi inashirikiana na wapelelezi wa jeshi na polisi kuangalia endapo wafunguwe mashitaka ya uasi dhidi ya Rais Yoon, kufuatia amri yake ya kijeshi aliyoitowa Disemba 3 na kutuma wanajeshi kulizunguka jengo la bunge linalotawaliwa na vyama vya upinzani.