1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi watawanya maandamano ya vijana Madagascar

1 Oktoba 2025

Polisi nchini Madagascar walitumia mabomu ya kutoa machozi na risasi za mpira kuwatawanya maelfu ya vijana waliokuwa wakiandamana Jumanne.

Antananarivo, Madagascar 2025 | Maandamano ya vijana
Vijana wanaandamana kupinga kukatika mara kwa mara kwa maji na umeme Picha: Zo Andrianjafy/REUTERS

Maandamano hayo yameendelea Madagasar, licha ya Rais Andry Rajoelina kuivunja serikali yake katika juhudi za kuzima machafuko nchini humo.  

Wakihamasishwa na maandamano ya vijana maarufu kama Gen Z ya Indonesia na Nepal, vuguvugu linaloongozwa na vijana kupinga utawala mbovu uliokita mizizi, limekasirishwa na kukatika mara kwa mara kwa maji na umeme katika taifa hilo kwenye Bahari ya Hindi.

Watu wanamtaka Rajoelina ajiuzulu

Maelfu waliandamana katika mji mkuu, Antananarivo kutokana na wito uliotolewa kupitia mitandao ya kijamii.

Umati mkubwa wa watu ulikuwa ukitamka maneno yanayomtaka Rajoelina aachie madaraka.

Maandamano yalianza kwa amani siku ya Alhamisi katika mji mkuu, Antananarivo, na tangu wakati huo yameenea hadi kwenye miji mingine.

Walioandaa maandamano hayo wamekanusha madai ya kuhusika katika uporaji na ghasia zilizozuka kando ya maandamano hayo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW