Polisi watumia mabomu ya machozi kutawanya waandamanaji DRC
20 Mei 2023Matangazo
Waandamaji kadhaa walikamatwa na askari wa usalama mara baada ya kuanza kwa maandamano hayo yaliyoitishwa na viongozi wa upinzani.
Viongozi hao ni pamoja na Martin Fayulu aliyeshika nafasi ya pili katika uchaguzi wa mwaka 2018 pamoja na mfanyabiashara na gavana wa zamani, Moise Katumbi .
Mbali ya suala la uandikishaji wapiga kura, waandamanaji wamekasirishwa na kupanda kwa gharama za maisha pamoja na ukosefu wa usalama wa muda mrefu katika eneo la mashariki mwa taifa hilo.
Waasi na makundi ya wabeba silaha wamekuwa wakifanya mashambulizi ambayo yamewauwa mamia ya watu kwenye eneo hilo na kusababisha wengine kuyakimbia makazi yao.