Polisi wavamia vyombo vya habari Zambia
16 Februari 2017Matangazo
Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kwamba badala yake polisi walimkamata mke wa Fred M'membe, mhariri mkuu wa gazeti la The Post, ambalo lilifungwa mwezi Juni. Watu walioshuhudia wamesema polisi walitumia nguvu kumkamata mke wa M'membe, Mutinta, na kwamba mwandishi habari Joan Chorwa alizuiwa kutoka katika nyumba hiyo wakati nyumba hiyo ilipovamiwa jana. Polisi wengine zaidi waliwasili katika nyumba hiyo leo. Uvamizi huo unafuatia hatua za M'membe kuweka pingamizi mahakamani dhidi ya kutaifishwa kwa mali za gazeti hilo la The Post, ambalo lilifungwa kwa misingi kwamba lilikuwa na deni la zaidi ya dola milioni 4 katika malipo ya kodi. Gazeti hilo halijafanya kazi tangu Novemba 2 mwaka jana, wakati lilipotakiwa kufilisiwa.