SiasaAsia
Polisi ya Korea Kusini yaombwa kumkamata rais Yoon
6 Januari 2025Matangazo
Timu ya wachunguzi wanaofanya kazi ya Upelelezi wa Rushwa kwa Viongozi wa Vyeo vya Juu (CIO) ilijaribu kutekeleza hati ya mahakama ya kumkamata Yoon siku ya Ijumaa baada ya kiongozi huyo kupuuza mara tatu wito wa kwenda kuhojiwa kutokana na jaribio lake la kuiweka nchi chini ya sheria ya kijeshi mnamoDesembatatu mwaka uliopita. Polisi nchini humo sasa wameombwa kutekeleza kibali hicho ingawa hata hivyo bado wataamua ikiwa watashirikiana na timu ya wachunguzi inayofanya upelelezi au la. Hapo jana, maelfu ya raia wa Korea Kusini waliandamana nje ya makazi ya Yoon mjini Seoul. Kambi moja ikitaka Yoon akamatwe huku nyingine ikitaka kushtakiwa kwake kutangazwe kuwa ni batili.