1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiUjerumani

Ujerumani yawakamata waliotaka kuipindua serikali

5 Novemba 2024

Polisi nchini Ujerumani wamewakamata washukiwa 8 wa kundi la wanamgambo wa mrengo wa kulia wanaoamini kwenye ubaguzi wa rangi, waliokuwa wanafanya mazoezi ya vita kwa ajili ya kuipindua serikali ya Ujerumani.

Ujerumani | Usalama | Polisi wakitekeleza majukumu yao
Polisi Ujerumani wakiwa kwenye majukumu yao.Picha: Christian Mang/REUTERS

Katika taarifa iliyotolewa leo, waendesha mashtaka wa shirikisho wamesema washukiwa hao ni sehemu ya shirika lililoundwa Novemba mwaka 2020 linaloitwa "Saechsische Separatisten" au wanaotaka kujitenga kutoka jimbo la Saxony.

Soma pia:Ujerumani inaweza kukabiliwa na uchaguzi wa mapema

Miongoni mwa waliokamatwa ni washukiwa 4 waasisi wa kundi hilo. Saba kati yao wamekamatwa katika miji ya mashariki mwa Ujerumani ya Leipzig, Dresden na Meissen. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW