Polisi yachunguza tukio la chuki dhidi ya wayahudi
23 Machi 2026
Polisi nchini Uingereza imesema inachunguza madai yaliyotolewa mtandaoni na kundi moja linalojifungamanisha na Iran, ya kuhusika na tukio la kuchomwa moto magari ya kubeba wagonjwa ya shirika moja la huduma za kujitolea la wayahudi nchini humo.
Kundi la Harakat Ashab al Yamin al Islamiya limedai leo Jumatatu, kupitia kanda ya video iliyoichapisha kwenye mtandao wa Telegram, kuhusika na tukio la kuyateketeza magari manne ya kubeba wagonjwa ya shirika la Hotzola, kikitajwa kuwa kitendo cha chuki dhidi ya wayahudi, lililolaaniwa na waziri mkuu Keir Starmer.
Polisi Uingereza iko tayari kukabiliana na vurugu za waandamanaji
Mkuu wa polisi kitengo cha uchunguzi, Luke Williams, amesema kitengo kinachohusika na shughuli za kupambana na ugaidi kinaongoza uchunguzi japo tukio hilo halikuhusishwa mara moja na ugaidi.
Watu watatu walionaswa kwenye kamera za CCTV wameonekana wakiyatia moto magari hayo leo asubuhi.