1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUingereza

Polisi yamsaka aliyeweka mabaki ya miili ya watu sandukuni

13 Julai 2024

Polisi nchini Uingereza inamsaka Yostin Andres Mosquera, raia wa Colombia anayehusishwa na mabaki ya ya miili ya watu wawili yaliyokutwa kwenye masanduku mawili mjini Bristol.

Polisi ya London
Polisi ya Uingereza inawatafuta watu wanaohusishwa na miili ya watu iliyotelekezwaPicha: Dan Kitwood/Getty Images

Polisi wanamtaja kijana huyo wa miaka 24, baada ya mabaki mengine kukutwa kwenye makazi yaliyoko Shepherd's Bush, kaskazini mwa London.

Jeshi hilo limesema maafisa walikuta mabaki ya miili kwenye nyumba hiyo jana Ijumaa, na wanaamini inahusiana na miili hiyo iliyokutwa kwenye masanduku yaliyotelekezwa karibu na Daraja la Clifton lililopo Bristol, kusini-magharibi mwa Uingereza siku ya Jumatano.

Jeshi la polisi aidha, limesema linaamini kuna watuhumiwa wengine wawili wanaume, ingawa bado hawajajulikana.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW