Pontida , Italia. Wanachama wa chama cha Northern league wanataka sarafu ya Lira itumike tena nchini humo.
19 Juni 2005Matangazo
Maelfu ya wanachama wa chama cha Northern League nchini Italy , chama kidogo kinachounda uongozi wa serikali ya waziri mkuu Silvio Berlusconi, leo kimepiga kura juu jinsi ya kuweka sawa kampeni ya chama hicho ya kutaka kurejesha sarafu ya Lira nchini Italy.
Waziri wa masuala ya jamii kutoka chama hicho Roberto Maroni ameanzisha kampeni hiyo mapema mwezi huu, akisema kuwa sarafu ya Euro imekuwa ni maafa kwa watumiaji pamoja na wafanyabiashara wadogo nchini humo.
Juhudi hizo limepuuziwa na vyombo vya habari kwa kusema chama hicho kinataka umaarufu wakati uchaguzi mkuu ukikaribia mwaka ujao.