1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa ateua makadinali wapaya 21

30 Septemba 2023

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis leo hii amewateua Makadinali wapya 21 katika hafla iliyofanyika katika uwanja wa Kanisa la Mtakatifu Petron mjini Vatican.

Katika hafla hiyo Papa aliwavisha makadinali hao kofia nyekundu, ambazo ni mahususi katika kuwatambua maafisa wapya wa kanisa hilo. Mmoja wa makadinali, Luis Pascual Dri wa Argentina mwenye umri wa miaka 95, hakuhudhuria hafla hiyo kutokana na chagamoto ya umri.Uteuzi wa baraza hilo la makardinali la Kanisa Katoliki, ambalo ndio huchagua mapapa wapya, huenda ukatoa nafasi kwa kiongozi huyo kuanzisha mchakato wa kumchagua mrithi wake.Hatua hii mpya ina maanisha kwamba makadinali 99 kati ya jumla ya 137 ambao kwa sasa wanauwezo wa kumchagua papa ajaye wameteuliwa na Papa Francis mwenyewe, mwenye umri wa miaka 86.