PORT AU PRINCE: Mafuriko yaua watu
13 Oktoba 2007Matangazo
Takriban watu 45 wameuwawa kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa nchini Haiti.
Mji wa Cabaret ulio kilomita 30 kaskazini mwa mji mkuu wa Port Au Prince ndio ulioathirika zaidi, miili ya watu 23 imeopolewa katika eneo hilo.
Takriban watu 1000 wamepoteza makaazi yao kufuatia mvua kubwa na mafuriko.
Hali ya tahadhari pia imetolewa katika nchi jirani za Nicaragua na Cuba.