1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Port-au-Prince:Kuachiliwa huru kwa Yvon Neptune.

28 Julai 2006

Waziri mkuu wa zamani wa Haiti Yvon Neptune, aliyekuwa amefungwa tangu mwaka 2004 kwa tuhuma za kuwauwa wapinzani wa rais wa zamani Jean Bertrand Aristide, ameachiliwa huru.

Tume ya Umoja wa Mataifa inayolinda utulivu nchini Haiti, imefurahishwa na kuachiliwa huru kwa Neptune mwenye umri wa miaka 60 ambae hali yake akiwa gerezani ilishadhoofika sana.

Yvon Neptune aliyekuwa Waziri Mkuu kuanzia mwaka 2001-2004, inaaminika kuwa ndie aliyepanga mbinu za mauwaji ya wapinzani 50 wa Aristide huko bandari ya magharibi ya mji wa Saint-Marc, wiki mbili kabla Aristide hajaondoshwa madarakani kwa nguvu mnamo mwezi February 2004.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW