Port – au – Prince.Polisi wauwa watu kadha katika mji mkuu wa Haiti.
5 Juni 2005Matangazo
Msako wa polisi dhidi ya magenge katika vitongoji wa mji mkuu wa Haiti Port – au – Prince huenda umesababisha vifo vya watu kadha, kwa mujibu wa watu walioshuhudia pamoja na madaktari.
Msemaji wa utawala wa umoja wa mataifa nchini humo amesema kuwa polisi wa Haiti wamesema watu wawili tu ndio waliokufa. Lakini wakaazi wamesema kuwa watu 18 wamepigwa risasi na kufa na kuwashutumu polisi kwa kuchoma nyumba kadha. Polisi wamekataa kutoa maelezo kuhusu msako huo.