1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PORT HARCOURT : Hali ya wasi wasi katika jimbo la Niger Delta

22 Septemba 2005

Mbabe wa vita wa Nigeria kutoka jimbo lenye kuzalisha mafuta la Niger Delta amehojiwa na polisi hapo jana kutokana na matamshi yake ya uhaini wakati wafuasi wake wakijimwaga mitaani na kutishia kufanya ghasia.

Kama hatua ya tahadhari kampuni ya Shell iliwarudisha nyumbani wafanyakazi wake kutoka makao yake makuu mjini Port Harcourt mji mkuu wa Niger Delta na kitovu cha kusafirisha nje mafuta.

Mamia ya wafuasi wa Mujahidi Dokubo- Asari waliziba barabara kuu ya mwendo wa kasi mjini Port Harcourt kwa mara kadhaa.Mamia ya polisi na wanajeshi baadae waliwatawanya kwa amani.

Kundi hilo la wafuasi wake lilitishia kufanya vurugu kubwa kutokana na kukamatwa kwa Asari hapo Jumanne na kuwaonya wafanyakazi wa mafuta kuondoka katika jimbo hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW