POTSDAM: Brazil na India zimetoka mkutanoni
22 Juni 2007Matangazo
Majadiliano ya kuregeza masharti ya biashara duniani yamevunjika.Majadiliano hayo,kati ya Umoja wa Ulaya,Marekani,Brazil na India mjini Potsdam,mashariki mwa Ujerumani,hayakuweza kuondosha tofauti kuu zilizopo kati ya pande hizo nne,kuhusu ushuru wa forodha na malipo ya ruzuku. Brazil na India zilitoka nje ya mkutano zikisema, majadiliano yao pamoja na Umoja wa Ulaya na Marekani hayafanyi maendeleo yo yote.Nchi zinazoendelea zinataka Umoja wa Ulaya na Marekani zipunguze ruzuku zinazotolewa kwa wakulima wao na badala yake,nchi zinazoendelea zitafungua masoko yake katika sekta za huduma na utengenezaji wa bidhaa.