1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Prabowo ajitangaza mshindi katika uchaguzi wa Indonesia

14 Februari 2024

Waziri wa ulinzi Prabowo Subianto, jenerali wa zamani aliyehusishwa na dhuluma za zamani za haki za binadamu, amedai kupata ushindi katika uchaguzi wa rais nchini Indonesia kulingana na matokeo ya kura yayiso rasmi.

Subianto ni jenerali wa zamani wa kijeshi katika utawala wa kidikteta wa Suharto
Prabowo Subianto amedai kupata ushindi katika uchaguzi wa rais wa IndonesiaPicha: Vincent Thian/AP Photo/picture alliance

Mgombea huyo mwenye umri wa miaka 72, ambaye wakati mmoja alipigwa marufuku na Marekani kukanyaga nchini humo kwa miongo miwili kutokana na rekodi yake ya haki za binaadamu, amewaambia maelfu ya wafuasi wake katika uwanja wa michezo wa mji mkuu Jakarta kuwa ushindi huo, kwa mujibu wa matokeo ya awali na yasiyo rasmi, ni ushindi wa Waindonesia wote. "Hesabu zote, watafiti wote wa maoni, wakiwemo watafiti wa wagombea wengine, wanaonyesha kuwa Prabowo na Gibran wameshinda katika duru ya kwanza."

Hakujawa na tamko la maafisa wa uchaguzi na magavana wawili wa zamani wa mikoa waliogombea pia katika uchaguzi huo wa taifa la tatu kubwa ulimwenguni, hawajakiri kushindwa.

Kwa mujibu wa matokeo yasiyo rasmi yaliyohesabiwa na mashirika ya utafiti ya Indonesia, Subianto ana kati ya asilimia 57 na 59 ya kura, huku zaidi ya asilimia 80 ya kura ikiwa imekwisha hesabiwa katika maeneo yaliyofanyiwa utafiti.

Rais anayeondoka Joko Widodo anatuhumiwa kwa kuiunga mkono kampeni ya Subianto kwa njia isiyofaa Picha: Mas Agung Wilis/AFP/Getty Images

Subianto amejionyesha kama mrithi wa rais wa sasa mwenye umaarufu mkubwa Joko Widodo, ambaye alimchagua mwanawe wa kiume kuwa mgombea mwenza. Alikuwa jenerali wa jeshi wakati wa utawala wa kidikteta wa Suharto.

Widodo anatengeneza "himaya ya kisiasa"

Wakosoaji wanamtuhumu Widodo kwa kujaribu kujenga himaya ya kisiasa licha ya kuwa rais wa kwanza aliyetoka nje ya tabaka maalum la kisiasa na kijeshi tangu kumalizika kwa utawala wa kiimla wa mwaka wa 1988 wa Suharto, ulioghubikwa na ukiukaji mkubwa wa haki za binaadamu, ubadhirifu na machafuko ya kisiasa. Yoes Kenawas, ni mchambuzi wa sasa "Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Indonesia kuwa rais aliyeko madarakani ana ndugu ambaye alishinda uchaguzi wa rais. Inaweza kusema kuwa himaya ya kisiasa ya Joko Widodo imeundwa katika ngazi ya juu kabisa ya serikali ya Indonesia”

Subianto aliachishwa kazi 1998 kama kamanda wa vikosi maalum vya Kopassus baada ya kutuhumiwa kuwateka nyara na kuwatesa wanasiasa waliompinga Suharto, ambaye wakati huo alikuwa baba mkwe wake.

Atakayechukua mikoba ya Widodo atarithi Uchumi wenye ukuaji mzuri na miradi kabambe ya miundo mbinu, ikiwemo uhamishnesiaji unaondelea wa mji mkuu wa taifa hilo kutoka Jakarta yenye msongamano mkubwa hadi kisiwa cha mpakani cha Borneo. Mradi mkubwa wa gharama ya dola bilioni 30.

Waindonesia walipiga kura leo katika uchaguzi uliofanyika kwa saa sita pekee kwenye nchi ya watu milioni 274. Uchaguzi huo pia una umuhimu mkubwa kwa Marekani na China kwa sababu Indonesia ina soko kubwa la ndani, maliasili kama vile nikeli na mafuta ya mawese, na ushawishi wa kidiplomasia na majirani zake wa Kusini mashariki mwa Asia.

afp, ap

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW