1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PRAGUE: Usalama umeimarishwa kufuatia onyo la shambulio

23 Septemba 2006

Polisi nchini Jamhuri ya Czech wamewatawanya askari wa ulinzi wenye silaha kati kati ya mji mkuu wa kihistoria,Prague,baada ya idara ya usalama kuonya juu ya uwezekano wa kufanywa shambulio la kigaidi.Waziri mkuu Mirek Topolanek amesema serikali ilikutana kupitisha uamuzi wa kuchukua hatua kali zaidi za usalama.Lakini hakueleza kitisho hicho ni cha aina gani.Jamhuri ya Czech ina kikosi kidogo nchini Afghanistan na vile vile polisi wa kijeshi wanatoa mafunzo nchini Irak.Jamhuri ya Czech,haikuwahi kulengwa kushambuliwa na magaidi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW