1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PRAGUE. Waziri mkuu wa Ucheki ashinda kura ya kutokuwa na imani naye.

1 Aprili 2005

Waziri mkuu wa jamhuri ya Ucheki, Stanislav Gross ameponea chupuchupu kura ya bunge ya kutokuwa na imani naye, kufuatia hatua ya wabunge wa kikomunisti kutoshiriki katika kura hiyo. Serikali ya mseto ilikumbwa na mzozo kuhusu fedha za kibinafsi za waziri mkuu huyo. Gross alikuwa na bahati ya mtende kwani kama si chama cha kikomunisti, angekuwa hayumo tena madarakani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW