1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PRETORIA: Mazungumzo ya Ivory Coast yaanza Afrika Kusini.

4 Aprili 2005

Mazungumzo ya amani ya Ivory Coast yameanza rasmi katika mji wa Pretoria chini ya uenyekiti wa rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini.

Mazungumzo hayo baina ya serikali ya Ivory Coast na wapinzani yamerejelewa tena tangu July mwaka uliopita.

Rais Thabo Mbeki alichaguliwa na Umoja wa Afrika kusimamia mazungumzo hayo yenye azma ya kumaliza uhasama baina ya makundi hayo mawili huku kukiwa na wasiwasi kuwa huenda vita vikaanza tena huko Ivory Coast.

Umoja wa nchi za Afrika unataka uhasama huo ukomeshwe kwani unaleta wasiwasi mwingi kwa bara la Afrika na ambao umesababisha kuzorota kwa kilimo cha cacao kutoka taifa hili lililoongoza kwa kilimo cha zao hilo duniani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW