Pretoria. Wachimba migodi Afrika kusini wakubali ongezeko la mshahara.
12 Agosti 2005Matangazo
Wachimba migodi ya dhahabu nchini Afrika kusini wamemaliza mgomo wao mkubwa kuwahi kuikumba sekta hiyo katika muda wa miaka 18.
Makubaliano na makampuni makubwa manne ya migodi yamekuja baada ya vyama vya wafanyakazi kukubaliana na malipo ya mishahara ambayo yana marupurupu zaidi.
Chama kikuu cha wachimba migodi pamoja na vyama vidogo vingine vimekubali ongezeko la mshahara la kati ya asilimia sita na saba.
Wachimba migodi wapatao 100,000 waligoma kufanya kazi kuanzia Jumapili jioni.
Halmashauri ya wauza madini nchini Afrika kusini inakadiria kuwa mgomo huo umeigharibu nchi hiyo inayozalisha dhahabu kwa wingi duniani kiasi cha Euro milioni 16 kwa siku.