PRETORIA:Afrika Kusini yaeleza kumaliza kazi ya upatanishi,Ivory Coast.
30 Agosti 2005Matangazo
Serikali ya Afrika Kusini imesema leo kuwa itatoa maelezo kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,kuwa imekamilisha kazi ya upatanishi nchini Ivory Coast na imetupa lawama kwa waasi na vyama vya siasa vya upinzani kwa kuchelewasha mchakato wa amani.
Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini,Aziz Pahad,wajibu wa msuluhishi kwa kiasi kikubwa kwa sasa umekamilika na akaonesha matumaini yake kuwa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika,wanajukumu sasa la kuhakikisha kuwa makubaliano yaliyofikiwa yanatekelezwa.