PRETORIA:Tony Blair aunga mkono juhudi za kutafuta suluhu ya Zimbabwe
1 Juni 2007Matangazo
Waziri Mkuu wa Uingereza anayeondoka Tony Blair anaunga mkono juhudi za Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini aliye mpatanishi katika tatizo la kisiasa na uchumi linalokumba nchi ya Zimbabwe.
Katika mkutano na waaandishi wa habari kiongozi huyo hakuelezea walichojadilia na mwenzake Rais Thabo Mbeki kuhusu Zimbabwe.
Rais Mbeki kwa upande wake hajaelezea juhudi ambazo zimefanyika katika kutafuta utatuzi wa suala hilo japo anapaswa kutoa ripoti kamili kwa Jumuiya ya SADC mwishoni mwa mwezi.
Waziri Mkuu Tony Blair aliyasema hayo alipokamilisha ziara yake ya mataifa matatu ya bara la Afrika ili kuliaga.