1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Prince Andrew wa Uingereza ajivua cheo cha kifalme

18 Oktoba 2025

Mwanamfalme wa Uingereza Prince Andrew ametangaza jana kuacha kutumia cheo chake cha kifalme cha Duke of York pamoja na heshima nyingine alizotunukiwa.

Mwanamfalme wa Uingereza Prince Andrew
Mwanamfalme wa Uingereza Prince AndrewPicha: Lindsey Parnaby/AFP

Mwanamfalme wa Uingereza Prince Andrew ametangaza jana kuacha kutumia cheo chake cha kifalme cha Duke of York pamoja na heshima nyingine alizotunukiwa. Hayo ni kufuatia uchunguzi mpya kuhusu uhusiano wake na Jeffrey Epstein aliyehukumiwa kwa uhalifu wa kingono.

Katika taarifa iliyotolewa na Kasri la Buckingham, Andrew alisema kuwa yeye na familia ya kifalme wamekubaliana kuwa tuhuma zinazoendelea dhidi yake zinatia doa kazi ya Mfalme na familia ya kifalme.

Tangazo hili linakuja wakati sehemu za kitabu cha kumbukumbu cha Virginia Roberts Giuffre zikianza kusambaa. Giuffre anadai alitekwa na Epstein na kulazimishwa kufanya ngono na Prince Andrew akiwa na umri wa miaka 17, madai ambayo Andrew ameyakana mara kwa mara.

Wachambuzi wa masuala ya kifalme wanasema uamuzi huu ni sehemu ya juhudi za kulinda heshima ya familia ya kifalme, hasa chini ya uongozi wa Mfalme Charles III.