Teknolojia ya tehama sasa inazidi kurahisisha mambo, huko Kenya imebuniwa program ya kutoa msaada wa kisheria katika nyanja mbalimbali.Mtumiaji anauchaguzi mpana anaweza kutumia kwa ujumbe, sauti na hata video, watumiaji wanasema haya ni mapinduzi makubwa ya teknolojia katika nyanja ya sheria.
Kurunzi ni video fupi ya DW Kiswahili inayomulika na kufafanua habari, matukio au masuala muhimu kwa lugha rahisi, picha zinazovutia na maelezo yanayomsaidia mtazamaji kuelewa kwa haraka.