1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pumzika kwa amani Diogo Jota

5 Julai 2025

Wachezaji wa Liverpool wameungana na familia na marafiki katika mazishi ya mchezaji Diogo Jota na kaka yake, siku mbili baada ya kaka hao kufariki katika ajali ya barabarani nchini Uhispania.

Portugal 2025 | Mazishi ya Diogo Jota
Majeneza ya Diogo Jota na kaka yake André Silva yakibebwa nje ya kanisa wakati wa mazishi yao huko Gondomar, karibu na Porto, Ureno.Picha: Manu Fernandez/AP Photo/picture alliance

Ibada ya mazishi ilifanyika katika kanisa la Igreja Matriz katika mji wa Gondomar, Ureno, ambako Jota alikuwa na makazi.

Kocha wa timu ya taifa ya Ureno, Roberto Martínez, pamoja na wachezaji kadhaa maarufu wa Ureno walihudhuria, wakiwemo Bernardo Silva na Rúben Dias wa Manchester City, na Bruno Fernandes wa Manchester United.

Wazazi wa marehemu walihudhuria ibada hiyo katika Kanisa la São Cosme, karibu na Porto, pamoja na Rais wa Ureno Marcelo Rebelo de Sousa, Waziri Mkuu Luís Montenegro, na wakala wa Jota.

Jota, mwenye umri wa miaka 28, na kaka yake André Silva, 25, walikutwa wamefariki karibu na mji wa Zamora, kaskazini-magharibi mwa Uhispania, mapema Alhamisi baada ya gari lao aina ya Lamborghini kupata ajali na kuwaka moto usiku wa manane.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW