1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Putin aelekea Vietnam akitokea Korea Kaskazini

19 Juni 2024

Vietnam inajiandaa kumpokea Rais Vladimir Putin wa Urusi aliyetarajiwa kuwasili Hanoi akitokea nchini Korea Kaskazini alikokutana na kutiliana saini mikataba ya ushirikiano na kiongozi wa huko, Kim Jong Un.

Korea Kaskazini Putin kwa Kim Jong Un
Msafara wa Rais Putin akiwa nchini Korea Kaskazini.Picha: GAVRIIL GRIGOROV/AFP/Getty Images

Putin anafanya ziara nchini Vietnam kutokana na mualiko wa Rais Nguyen Phu Trong.

Siku ya Jumatano (Juni 20) rais huyo wa Urusi alitarajiwa kushiriki hafla rasmi katika kasri la rais kabla kufanya mazungumzo na Rais Trong ambaye pia ndiye katibu mkuu wa Chama cha Kisoshalisti cha Vietnam.

Soma zaidi: Korea K., Urusi zasaini mkataba wa ushirikiano wa kimkakati

Putin alipangiwa pia kukutana na Waziri Mkuu wa Vietnam, Pham Minh Chinh, ambaye alisomea Urusi.

Baada ya kutengwa katika jukwaa la kimataifa, Putin anatafuta uungwaji mkono kutoka kwa marafiki waliosalia wa Urusi.

Haijakuwa wazi bado jinsi Vietnam inavyotazamia kunufaika na ziara ya Putin ambaye bado kuna waranti wa kumkamata uliotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW