1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Putin afanya mazungumzo ya nadra na Waziri Mkuu wa Slovakia

23 Desemba 2024

Rais wa Urusi amekuwa mwenyeji wa Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico katika ziara ya nadra ya kiongozi huyo wa Umoja wa Ulaya katika ikulu ya Kremlin tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mnamo Februari mwaka 2022.

Urusi | 2024 | Slovakia| Kremlin
Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico na Rais wa Urusi Vladimir Putin katika mkutano wa pamoja Ikulu ya KremlinPicha: Artyom Geodakyan/TASS/IMAGO

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov ameliambia shirika la habari la Urusi RIA kuwa Waziri Mkuu huyo wa Slovakia aliwasili Urusi kwa ziara ya kikazi na alikutana na Putin jana jioni.

Kulingana na Peskov, mazungumzo kati ya viongozi hao wawili yalijikita juu ya masuala ya "hali ilivyo kimataifa” na usambazaji wa gesi asilia ya Urusi.

Fico aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook baada ya kukutana na Putin kwamba, aliwaeleza viongozi wa Umoja wa Ulaya kuhusu ziara yake mjini Moscow.

Soma pia: Ukraine yasema wanajeshi wengi wa Korea Kaskazini wameuawa Kursk 

Gesi asilia ya Urusi bado inasafarishwa kuelekea baadhi ya nchi za Ulaya, ikiwemo Slovakia, kupitia Ukraine kwa mujibu wa makubaliano ya miaka mitano yaliyotiwa saini kabla ya vita na ambayo yanatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwaka huu.

Viongozi hao wawili walijadili pia juu ya "uwezekano wa mapema na kwa njia ya amani ya kuvimaliza vita hivyo” na uhusiano kati ya Urusi na Slovakia, Fico aliandika kwenye mtandao wake wa Facebook.

Slovakia na Hungary, ambazo zote zinategemea gesi ya Urusi, zimeibua wasiwasi kuhusu uwezekano wa usambazaji wa gesi hiyo kukatizwa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW