Putin afanya ziara nchini Vietnam
20 Juni 2024Rais wa Urusi Vladimir Putin amewasili mjini Hanoi nchini Vietnam kwa ziara ya kiserikali kufuatia mkutano na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un. Hayo yameripotiwa na afisi ya rais wa Urusi.
Putin anafanya ziara katika mji mkuu wa Vietman kufuatia mualiko wa Mkuu wa chama cha Kikomunisti Nguyen Phu Trong. Rais Putin amewasili Hanoi akitokea Korea Kaskazini alikoondoka jana jioni baada ya kufanya ziara ya siku mbili.
Hivi leo Putin atashiriki hafla ya kukaribishwa katika ikulu ya rais kabla kuhudhuria mazungumzo ya pande mbili na mkuu wa chama cha kikomunisti Trong.
Soma pia: Rais Putin anazuru mji wa Hanoi
Putin pia atakutana na waziri mkuu wa Vietnam Pham Minh Chinh na raia wa Vietnam waliosomea nchini Urusi. Putin pia atahudhuria dhifa ya kitaifa.