1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Putin aionya Marekani kuipatia Ukraine makombora ya Tomahawk

5 Oktoba 2025

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema ikiwa Marekani itaipatia Ukraine makombora ya Tomahawk ili kufanya mashambulizi ya masafa marefu ndani ya nchi yake, hilo litapelekea kuvunjika kwa uhusiano kati ya mataifa hayo.

Sochi I Rais wa Urusi Vladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir Putin akiwa katika mjadala huko SochiPicha: Mikhail Metzel/Sputnik/REUTERS

Siku ya Alhamisi, Putin alisema Ukraine haiwezi kutumia makombora hayo bila ushiriki wa moja kwa moja wa wanajeshi la Marekani akionya kuwa usambazaji wowote wa makombora hayo utachukuliwa kama hatua ya kuuchochea mzozo huo.

Viongozi hao wawili wamekuwa wakirushiana maneno katika siku za hivi karibuni ambapo Trump alimuita  Putin  kuwa "chui wa karatasi" kwa kushindwa kumaliza vita Ukraine, huku Putin akisema kuwa NATO ndio wanaopaswa kuitwa hivo kwa kushindwa kuzuia mafanikio yake katika uwanja wa vita. Hayo yakiarifiwa, vita vinaendelea ambapo watu watano wameripotiwa kuuawa nchini Ukraine kufuatia mashambulizi ya makombora na droni ya Urusi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW