1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin aionya Poland isipeleka wanajeshi mpakani na Belarus

22 Julai 2023

Rais Vladimir Putin wa Urusi ameionya Poland dhidi ya uamuzi wake wa kupeleka tena vikosi vya jeshi kwenye mpaka wake na taifa jirani la Belarus iliyo mshirika mkubwa wa utawala mjini Moscow.

Russland Präsident Putin in Moskau
Rais wa Urusi, Vadimir PutinPicha: Russian President Press Office/dpa/picture alliance

Putin amesema Belarus ni taifa muhimu kwa Urusi na mpango wowote wa kuitisha nchi hiyo utajibiwa vikali na Moscow. Kiongozi huyo wa Urusi alikuwa akizungumza mbele ya kikao cha Baraza la Usalama wa Taifa jana Ijumaa.

Matamshi yake yanafuatia uamuzi wa Poland uliotangazwa jana, wa kupeleka idadi ya wanajeshi ambayo bado haijulikani kwenye mpaka wake wa mashariki.

Soma zaidi: Mzozo kati ya Poland na Belarus kuendelea kwa miezi kadhaa

Poland ambayo ni mwanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO imesema uamuzi huo unatokana na uwepo wa wapiganaji wa kundi la mamluki wa Urusi la Wagner kwenye taifa jirani la Belarus.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW