1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin apongeza Afrika inavyoshughulikia masuala ya kimataifa

29 Julai 2023

Rais wa Urusi Vladimir Putin amewasifu viongozi wa Afrika katika mkutano wa kilele hapo jana, na kupongeza jukumu la bara hilo katika kushughulikia masuala ya kimataifa.

Rais wa Urusi Vladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Pavel Bednyakov/POOL/AFP/Getty Images

Katika mkutano huo wa kilele, Rais Putin ameahidi kupanua mahusiano ya kisiasa na kibiashara na bara hilo.

Akihutubia mkutano wa kilele wa Urusi na viongozi wa Afrika kwa siku ya pili mjini Saint Peterburg, Putin amesema Urusi itachambua kwa karibu pendekezo la amani kwa Ukraine ambalo viongozi wa Afrika wanataka kulifuata.

Soma zaidi: Putin asema Urusi imetia saini makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi na zaidi ya nchi 40 za Afrika

Ameongeza kuwa hilo ni suala kubwa na hawataepuka kulizingatia akisisitiza kuwa serikali yake inalichukulia pendekezo hilo kwa heshima na umakini.

Putin pia amewahimiza viongozi hao kuzungumza na Ukraine ambayo imekataa kushiriki katika mazungumzo hadi Urusi itakapoondoa vikosi vyake nchini humo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW