1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Putin aipongeza Korea Kaskazini kwa msaada wake katika vita

18 Juni 2024

Rais Vladimir Putin aipongeza Korea Kaskazini kwa kuiunga mkono kwenye vita dhidi ya Urusi dhidi ya Ukraine.

Russland Nordkorea Gipfel in Wladiwostok | Kim Jong Un und Putin
Picha: Alexander Zemlianichenko/AP Photo/picture alliance

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameipongeza Korea Kaskazini kwa msaada wake katika vita vya Urusi dhidi ya Ukraine. Amesema hayo kabla ya ziara yake nchini humo baadaye Jumanne.

Putin amesifu hatua ya kutolewa kwa msaada huo mkubwa katika barua yake iliyochapishwa kwenye gazeti rasmi la Rodong Sinmun la mjini Pyongyang.

Kulingana na Putin, nchi zote mbili zina mipango ya kushirikiana, kujenga usanifu wa usalama ndani ya Muungano wa Wakuu wa Majeshi ya Korea Kaskazini, kukabiliana na Magharibi vikwazo, na kuanzisha mifumo huru ya miamala.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW