1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin akabiliwa na miito ya amani kwa vita vyake na Ukraine

23 Oktoba 2024

Viongozi wa ulimwengu wametoa wito wa amani katika Mashariki ya Kati na Ukraine katika mkutano wa kilele wa BRICS nchini Urusi leo.

Russland Kazan Brics Treffen | Modi Putin und Xi
Rais Xi Jinping wa China, Rais wa Urusi Vladimir Putin, Waziri Mkuu wa India Narendra Modi wakihudhuria mkutano wa 16 wa wakuu wa nchi za BRICS huko Kazan.Picha: Alexander Shcherbak/Tass/IMAGO

Rais wa Urusi Vladimir Putin ambaye ndio mwenyeji wa mkutano huo amewaambia washiriki kuwa anakaribisha maombi ya wanaotaka kuwa wapatanishi katika mzozo wa Ukraine. Mkutano huo wa karibu viongozi 20 wa ulimwengu katika mji wa Kazan, ndilo jukwaa kubwa kabisa la kidiplomasia kuandaliwa Urusi tanguPutinalipoamuru wanajeshi kuivamia Ukraine mwaka wa 2022. Rais wa China Xi Jinping ameuambia mkutano huo wa kilele kuwa lazima mapigano yasitishwe nchini Ukraine. Waziri Mkuu wa India Narendra Modi pia ametoa wito wa amani. Kuhusu Mashariki ya Kati, Rais wa Iran Masoud Pezeshkian amewahimiza wanachama wa BRICS kutumia uwezo wao wote wa pamoja na kibinafsi kumaliza vita katika Ukanda wa Gaza na nchini Lebanon. Rais wa Brazil Luiz Inacio Lila da Silva pia ametoa wito wa kupunguzwa mvutano Mashariki ya Kati nchini Ukraine.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW