1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin akubali pendekezo la China kwa mzozo wa Ukraine

16 Oktoba 2023

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema pendekezo la China kuhusu mazungumzo ya amani na Ukraine linaweza kuwa msingi wa makubaliano ya amani.

20th Annual Meeting of Valdai Discussion Club
Picha: Vladimir Smirnov/TASS/dpa/picture alliance

Hayo ni kulingana na mahojiano aliyoyafanya na televisheni ya China na mbayo yamechapishwa leo na ikulu ya Kremlin.

Putin ameishutumu pia Ukraine kwa kutokuwa na nia ya kushiriki mazungumzo hayo ya amani.

Lakini serikali ya Kyiv imekuwa mara kadhaa ikitoa sharti la kuondoka kwanza kwa vikosi vya Urusi katika ardhi yake kabla ya kuanza mchakato wowote wa mazungumzo.

Soma: Kishida awasili Kyiv wakati Xi akikutana na Putin Moscow

Rais huyo wa Urusi anatazamiwa kusafiri hadi Beijing siku ya Jumanne (Oktoba 17) kukutana mwenzake wa China, Xi Jinping, na kuhudhuria mkutano wa kilele unaolenga kujadili maendeleo yaliyofikiwa na China katika miradi ya miundombinu kimataifa.

Xi na Putin wanatarajiwa pia kujadili masuala mbalimbali ikiwemo mzozo unaoendelea Mashariki ya Kati.