1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin akutana na viongozi wa Afrika

27 Julai 2023

Mkutano wa kilele kati ya Urusi na Afrika unaanza leo, ambapo Rais Vladmir Putin anapanga kuimarisha ushirikiano na mataifa ya Afrika wakati huu nchi yake ikikabiliwa na vikwazo vya kimataifa kwa uvamizi wa Ukraine.

Russland-Afrika-Gipfel in Sotschi 2019
Picha: Valery Sharifulin/Tass/dpa/picture alliance

Katika barua yake ya kuwakaribisha washiriki, Putin amesema kuwa ushirikiano wa biashara, uwekezaji, nishati, kupunguza umasikini, kuhakikisha usalama wa chakula na mabadiliko ya tabianchi, vitajadiliwa katika mkutano huo wa kilele. 

Putin pia anapanga kukutana na viongozi wa Afrika na kuendeleza mazungumzo kuhusu juhudi za mpango wa amani zinazofanywa na Afrika kwa ajili ya Ukraine.

Soma zaidi: Afrika Kusini yasifia ujumbe wa amani Ukraine baada ya mazungumzo

Ujumbe wa Afrika wakutana na Putin kuhusu mzozo wa Ukraine

Imeripotiwa kuwa wawakilishi kutoka nchi 49 kati ya 54 za Afrika watahudhuria mkutano huo unaofanyika St. Petersburg, ambapo 17 ni wakuu wa nchi na serikali.

Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba, anaizuru Liberia, ikiwa ni ziara yake ya tatu barani Afrika tangu Urusi ilipoivamia nchi yake mnamo Februari 2022.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW