1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin akutana na wajumbe wa Marekani, Moscow

23 Januari 2026

Ikulu ya Kremlin imesema kuwa mazungumzo ya usiku wa kuamkia leo kati ya Rais Vladimir Putin na Mjumbe wa Marekani Steve Witkoff yalikuwa "yenye umuhimu kwa kila njia."

Rais wa Urusi Vladimir Putin na Mjumbe wa Marekani Steve Witkoff mjini Moscow
Rais wa Urusi Vladimir Putin na Mjumbe wa Marekani Steve Witkoff mjini MoscowPicha: Alexander Kazakov/Sputnik/Kremlin Pool Photo via AP/dpa/picture alliance

Mshauri wa kidiplomasia wa Kremlin Yuri Ushakov amesema maafisa wa Ukraine, Marekani na Urusi watakutana huko Falme za Kiarabu kwa majadiliano zaidi hii leo.

Putin na wajumbe wa Marekani Steve Witkoff na Jared Kushner, walikutana na muda mchache kabla saa sita usiku wa kuamkia leo baada ya Rais Donald Trump kusema makubaliano ya kusitisha vita vya Ukraine yako karibu sana kufikiwa huku Witkoff akisema ni suala moja tu lililosalia kupatiwa mwafaka.

Haya yanafanyika wakati ambapo Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amesema amefikia makubaliano ya kupata msaada wa mifumo mpya ya ulinzi wa angani katika Jukwaa la Kiuchumi Duniani.

Zelenskiy vile vile amewashambulia washirika wake wa Ulaya kwa kile alichosema ni hatua yao ya taratibu ya kukabiliana na uvamizi wa Urusi nchini mwake.

Zelenskiy amesema kuwa "Ulaya imepotea."

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW